UPINZANI: IEBC KIBARAKA WA SERIKALI
Muungano wa upinzani umeibua madai kwamba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ni kibaraka wa serikali, ukirejelea chaguzi ndogo zilizopita ambazo muungano huo umesema zilifichua uhusiano kati ya IEBC na serikali ya Kenya Kwanza.
Viongozi wa muungano huo akiwemo Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua na Eugene Wamalwa, wameionya tume hiyo inayoongozwa na Erastus Ethekon dhidi ya kuvuruga uchaguzi mkuu ujao, wakiapa kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa maeneo bunge la Malava na Mbeere North.
Wameapa kutokubali kugawanywa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































