#Football #Sports

CARABAO YAINGIA RAUNDI YA 4

Kipute cha Carabao kinaingia raundi ya 4 hii leo huku timu kama vile Manchester United, Everton na Aston Villa zikiwa zimebanduliwa nje ya mashindano hayo, nazo timu 5 pekee zilizo nje ya ligi kuu ziisalia.

Klabu ya Grimsby Town inayoshiriki League 2 imekuwa kitovu cha gumzo kwenye mashindano hayo kufikia sasa, baada ya kuwabandua Manchester United katika raundi ya 2 kabla ya kuwabandua Shefield Wednesday, na sasa watamenyana na Brentford hii leo.

Fulham watasafiri kupambana na Wycombe inayoshiriki Legaue 1.

Hapo kesho, jumla ya mechi 9 zitasakatwa, mabingwa watetezi Newcastle United wakiwakaribisha Tottenham, Arsenal vs Brighton, Man City wakiwatembelea Swansea City nao Wolves wamalize udhia dhidi ya Chelsea ugani Molineux.

Crystal Palace watakuwa wageni wa Liverpool, wakiwa tayari wamepambana mara 2 msimu huu, Palace wakiibuka na ushindi katika Community Shield na katika ligi kuu, na watalenga kuwalaza mabingwa hao wa EPL kwa mara ya 3 msimu huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CARABAO YAINGIA RAUNDI YA 4

DROO YA CAF CONFEDERATIONS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *