ARSENAL WAPOTEZA NAFASI YA KIPEKEE
Viongozi wa ligii ya soka nchini Uingereza, EPL, Arsenal, walipoteza nafasi ya kupanua mwanya wa pointi 8 uongozini mwa ligi hiyo baada ya kutoa sare ya kutofungana dhidi ya Liverpool ugani Emirates Stadium.
The reds ni mojawapo ya timu 2 pekee ambazo zimefanikiwa kuwacharaza vijana wa Mikel Arteta msimu huu, na walikaribia kuikabidhi kichapo cha 3 jana usiku kupitia kwa beki wa wing’i ya kulia Conor Bradley aliyegonga chuma.
Arsenal walishindwa kufunga bao nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu, ila wakafanya kila wawezalo kuongeza mwanya wa uongozi na kufanikiwa kusonga mbele ya Manchester City na uongozi wa pointi 6.
Sare 3 mfululizo kwa City ziliipa Arsenal fursa ya kutwaa taji la EPL baada ya kusubiri kwa miaka 22, ila sare ya jana huenda ikawa laiti tungalishinda Liverpool kwa Arsenal mwishoni mwa msimu.
Arteta alimwandoa Viktor Gyokeres kunako dakika ya 64 akiwa hana shoti yoyote licha ya krosi nyingi zilizopita kwenye kijisanduku bila kumaliziwa, na kuwaleta Gagriel Jesus, Noni Madueke na Eberechi Eze ila bado miti ikawa telezi.
Pointi moja inawaacha Liverpool katika nafasi ya 4, pointi 1 juu ya Newcastle United na Manchester United wanaposaka kupata fursa ya kushiriki kipute cha klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































