EACC YAREJESHA ARDHI YA WAZIRI KARURA
Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imeimarisha vita dhidi ya unyakuzi wa ardhi nchini, baada ya kufanikiwa kurejesha vipande kadhaa vya ardhi vyenye thamani ya mabilioni ya pesa katika maeneo mbali mbali nchini.
Ya hivi punde ni ardhi ya umma yenye ekari 17 katika msitu wa Karura, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.8, ambayo unyakuzi wake ulihusishwa na Waziri wa zamani JJ Kamotho.
Mahakama ya ardhi na mazingira imeagiza kufunguliwa mashtaka maafisa wawili wa ardhi waliohusishwa na unyakuzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































