KPA YANG’ARA KWENYE MASHINDANO YA FIBA ZONE FIVE WBLA2025
Kocha mkuu wa Kenya Ports Authority (KPA), Anthony Ojukwu,
amesema hatima ya timu hiyo katika mashindano ya kufuzu kwa FIBA
Zone Five Women’s Basketball League Africa (WBLA) 2025 imo
mikononi mwao, huku akiwataka wachezaji wake kutochukulia mechi
yoyote kwa urahisi.
Timu hiyo ya Mombasa, ambayo ilinyakua nishani ya fedha mwaka
2023, imeanza kampeni zake kwa nguvu katika Ukumbi wa Nyayo
Gymnasium.
KPA ilianza vyema kwa ushindi wa 81–57, ikafuatia kwa kuilaza Magic
Stormers ya Uganda kwa 94–41, kabla ya kuizima Gladiators ya
Burundi kwa ushindi mnono wa 100–42 katika mechi yao ya tatu ya
Kundi A siku ya Alhamisi.
Ojukwu amesema wachezaji wake wameonesha ari na umoja wa hali
ya juu, akisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha Kenya inawakilishwa
vyema kwenye hatua ya mwisho ya WBLA 2025.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































