KIPCHOGE AJIANDAA KWA HISTORIA MAREKANI
Bingwa mara 2 katika michezo ya Olimpiki Eliud Kipchoge amesema ana malengo anayotaka kuafikia anapojiandaa kuishiriki mbio za New York City Marathon Jumapili hii kwa mara ya kwanza.
New York City, ama The Big Apple jinsi inavyofahamika, ndilo jiji pekee jipya ambako Kipchoge hajashiriki mbio katika safari yake ya miaka 12 ya riadha iliyoshuhudia akivunja na kuweka rekodi katika mbio kuu za Marathon katika miji kama vile Berlin Tokyo, London na Chicago.
Kipchoge, anayesisitiza kwamba hana chochote anachotaka kumwonyesha yeyote katika riadha, anasema lengo lake kutia juhudi zake zote katika mbio hizo.
Mwanariadha huyo anayechukuliwa kuwa bora zaidi wa mbio za marathoni katika historia atakimbia mbio kuu za marathoni kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja kwa mara ya kwanza katika taaluma yake.
Ataingia mbio hizo baada ya kumaliza wa 9 katika mbio za Sydney Marathon, ambazo zilijiri miezi michache baada ya kumaliza wa 6 katika mbio za London Marathon
Hata hivyo, bingwa huyo mara 5 wa mbio za Berlin Marathon anasema ana matumaini ya kufanya vyema katika jiji la New York kwa mara ya kwanza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































