MURKOMEN: TOA HONGO UKAMATWE
Vijana wanaolenga kujiunga na vikosi vya polisi kwenye usajili ambao umeratibiwa wiki ijayo wamehakikishiwa kwamba zoezi hilo litaendeshwa kwa uwazi na usawa na watakaopatikana wakijihusisha na ufisadi watawajibishwa kisheria.
Akizungumza katika kaunti ya Bomet, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amewataka wananchi kuwaripoti watakaohusika na visa hivyo ili kuhakikisha uadilifu wa zoezi la usajili wa makurutu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































