#Football #Sports

KPL YAENDELEA LEO ULINZI IKILENGA KUJIKWAMUA

Ligi kuu ya soka nchini KPL inaendelea hii leo kwa mechi za katikati ya wiki, ambapo mechi moja imeratibiwa kusakatwa.

KCB FC watalenga kupata ushindi katika mechi 2 mtawalia baada ya kusuasua, watakapomenyana na Ulinzi Stars majira ya saa kumi alasiri.

Kwa upande wao, Ulinzi watalenga kupata ushindi wa kwanza katika mechi 3 baada ya kuandikisha sare na kupoteza katika mechi 2 zilizopita za ligi.

Wanabenki wamo katika nafasi ya 8 kwa pointi 15, nao wanajeshi wakiwa katika nafasi ya 11 kwa pointi 13.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KPL YAENDELEA LEO ULINZI IKILENGA KUJIKWAMUA

CITY WAWATOA MADRID RANGI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *