#Local News

UHALALI WA JOPO LA KUTIMULIWA KWA GACHAGUA KUBAINIKA

Mahakama ya upeo imeratibiwa hii leo kutoa uamuzi wake kubaini iwapo jopo la mahakama kuu lililoteuliwa kusikiliza kesi ya akubanduliwa afisini kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua lilibuniwa kikatiba.

Jopo la majaji 4 wa mahamama hiyo ya upeo litatoa uamuzi kuhusu jopo la majaji 3 wa mahakama kuu lililosikiliza na kuamua kwamba Gachagua atimuliwe Oktoba mwaka 2024.

Miongoni mwa utata kwenye kesi hiyo ni iwapo naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu alizingatia katiba katika kubuni jopo hilo kwa niaba ya Jaji Mkuu Martha Koome.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *