AKONNOR ASHUSHA PUMZI KUFUATIA USHINDI
Meneja wa Gor Mahia Charles Akonnor ameonyesha kupata afueni baada ya vijana wake kupata ushindi wa kwanza katika mechi 4 kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wa ligi kuu ya KPL Kakamega Home Boyz.
Bao la pekee la Alpha Onyango katika dakika ya 19 lilitosha kuwapa K’Ogalo ushindi muhimu na kuwawezesha kufungua pengo la pointi 2 kileleni mwa jedwali.
Gor sasa wana pointi 23, 2 mbele ya KCB FC, Police FC, Tusker FC na Posta Rangers ambao wanatenganishwa tu na ubora wa mabao ila wote wana pointi 21.
Ushindi huo ulijiri baada ya Gor kumaliza mechi 3 bila ushindi, kikiwemo kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya APS Bomet, 1-0 dhidi ya AFC Leopards na sare ya kutofungana dhidi ya Bandari FC.
Hata hivyo, Akonnor ameridhishwa na matokeo ya jana, akitumai ni mwanzo wa kuweka nyuma masaibu yao.
Ligi hiyo inaendelea hii leo ambao Kariobangi Sharks watachuana na Bidco United, huku Polisi FC wakilenga kutetea taji lao dhidi ya Murang’a Seal ugani St Sebastian Park, huku AFC Leopards wakivamia ngome ya Ulinzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































