WANAHARAKATI WATAKA KUACHIWA KWA WENZAO
Mashirika ya kutetea haki nchini yameendelea kuzishinikiza serikali za Uganda na Kenya kuharakisha na kuwarejesha nchini wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo walioripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Miongoni mwa mashirika hayo ni chama cha wanasheria LSK, Amnesty International na Haki Africa, yakisema hali ya afya ya wawili hao imezorota.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































