MIMI NDIO SIFUNA KITENGELA!
Viongozi wa chama cha ODM wanaoegemea mrengo wa katibu mkuu Edwin Sifuna wametangaza kumuunga mkono Sifuna kupinga ushirikiano wa kisiasa kati ya ODM na chama tawala cha UDA kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Viongozi hao akiwemo naibu kinara Godfrey Osotsi ambaye ni seneta wa Vihiga, gavana wa Siaya James Orengo na mbunge wa Embakasi East Babu Owino, walikuwa wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado, wakipuzilia mbali uwezekano wa kufurushwa kutoka uongozi wa bunge kutokana na msimamo wao.
Mkutano huo hata hivyo ulikatizwa ghafla baada ya polisi kuutawanya umati.
Jicho Pevu kuwania ugavana Mombasa
Mgombea wa ugavana katika kaunti ya Mombasa atakayepeperusha bendera ya muungano wa upinzani atakauwa mbunge wa Nyali Mohammed Ali.
Haya ni kulingana na chama cha DCP kinachoongozwa na Rigathi Gachagua, kikisema muungano huo utamwishinisha Ali ila chama atakachotumia kitawekwa wazi baadaye.
Mbunge huyo alikigura chama cha UDA kwa madai kwamba kinahujumu azma yake ya kuwania ugavana mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































