NAIROBI UNITED ‘WATAMANI KUSAHAU’ MWANZO CAF
Klabu ya Nairobi United ilianza vibaya awamu ya makundi ya mechi ya mashirikisho ya CAF Confederations, baada ya kutandikwa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco ugani Stade V Mohammed jana usiku.
Naibois waliokuwa wakicheza mechi yao kwanza kabisa katika awamu ya makundi baada ya kufanya vyema katika mechi za ufunguzi, walizidiwa nguvu, kasi, tajriba na maarifa, wakikubali kufungwa ndani ya dakika 3 za ufunguzi kupitia kwa Ayoub Bouchta ambaye shuti lake liliteleza mikononi mwa kipa Kevin Oduor na kujaa wavuni.
Mabingwa hao wa FKF Cup walikaza kamba wakilenga kurejea mchezoni, ila wakashindwa kustahimili vishindo na kuporomoka tena mwishoni mwa kipindi cha kwanza, Mohammed Bouchoura akifunga bao la pili, bao hilo likijiri baada ya Shami Kibwana kupoteza nafasi ya wazi.
Mohammed Rahyi aligongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza, na kuzidisha mwanya wa tajriba baina ya kalbu hizo 2.
Nairobi United watahitaji kujikusanya ten ana kuwakabili AS Maniema kwenye mechi yao ya 2 ya Group B, Maniema wakiwa katika nafasi ya 2 baada ya kuwanyuga Azam 2 mtungi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































