#Local News

RUTO AHIMIZA MAZUNGUMZO KUOKOA HALI UARABUNI

Rais William Ruto ameshutumu mashambulizi ya makombora yanayolenga ngome za kijeshi katika mataifa yaliyo mashariki ya kati huku vita vikichacha katika eneo hilo.

Haya yanajiri baada ya Iran, katika kulipiza kisasi dhidi ya uvamizi wa Amerika na Israel, kulenga ngome hizo katika mataifa ya United Arab Emirates, Qatar, Saudi Arabia, Oman, Iraq, Jordan, Kuwait na Bahrain.

Kupitia taarifa, Ruto amesema vita hivyo vinatishia usalama wa kimataifa, akihimiza mazungumzo yatakayopelekea kusitishwa kwa vita hivyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *