CARRICK ATEULIWA KUINOA UNITED
Manchester United imemteua Michael Carrick kama meneja mshikilizi hadi mwisho wa msimu kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim, akitwikwa jukumu la kuwarejesha United kwenye dimba la klabu bingwa barani Ulaya.
Carrick mwenye umri wa miaka 44, alishinda mataji 12 makuu na klabu hiyo katika kipindi cha miaka 12 alichoichezea.
Kiungo huyo wa zamani aliwahi kuiongoza United kwa mechi 3 bila kupoteza mwaka 2021 alipoteuliwa kushikilia wadhifa huo, kabla ya kutwaa ukocha wake wa kwanza katika klabu ya Middlesbrough.
Hata hivyo, alifutwa kazi Juni mwaka jana baada ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 10 kwenye ligi ya Championships, na sasa anachukua uongozi wa United walio katika nafasi ya 7.
Kibarua chake cha kwanza kitakuwa dhidi ya Manchester City Jumapili hii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































