#Football #Sports

XABI ALONSO ASEMA REAL MADRID ITAREJESHA UBORA

Kocha wa Real Madrid anayekumbwa na presha, Xabi Alonso, amesema hali anayopitia inaweza kubadilika haraka kabla ya mchezo wao muhimu wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City

Madrid imeshinda mechi mbili pekee kati ya saba zilizopita katika mashindano yote, ikipoteza 2–0 dhidi ya Celta Vigo huku ripoti za Uhispania zikidai kuwa Alonso anaweza kufutwa kazi endapo atashindwa na kikosi cha Pep Guardiola.

Alonso amesema wachezaji wake wanaamini wanaweza kushinda Man City katika uwanja wa Bernabeu na kujiimarisha kwenye msimamo wa awamu ya ligi, ambako kwa sasa wapo nafasi ya tano.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

XABI ALONSO ASEMA REAL MADRID ITAREJESHA UBORA

WACHEZAJI WA MISRI WAMUUNGA MKONO SALAH

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *