#Football #Sports

LINDAH KIHARA NGUZO YA KAYOLE STARLETS, MKUFUNZI

Kocha mkuu wa klabu ya Kayole Starlets inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Mary Adhiambo, amemtaja mshambulizi wa klabu hiyo Lindah Kihara kama nguzo kwa timu hiyo, kutokana na mchezo wake wa kufana msimu huu.

Fowadi huyo amekuwa katika ubora wake, akifunga mabao 3 na kuchangia bao 1 katika mechi 6 za ligi, mchango ambao umeipiga jeki azma ya klabu hiyo kutwaa taji la FKF-WPL.

Adhiambo ametaja uwezo wa fowadi huyo wa kumalizia mbeleya lango na kujitolea kwake katika mazoezi kama baadhi ya vitu ambavyo vimemweka katikahali hiyo.

Aidha, amesema kikosi chake kimejiandaa kisawasawa kumenyana na Ulinzi Starlets wikendi hii.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

LINDAH KIHARA NGUZO YA KAYOLE STARLETS, MKUFUNZI

NDAKWA AAHIDI USHIRIKIANO

LINDAH KIHARA NGUZO YA KAYOLE STARLETS, MKUFUNZI

SERIKALI KUWAZADI MAGWJI WA DEAFLYMPICS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *