ICHUNG’WA AMUENZI JOHANA NG’ENO
Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung’wa, amemuenzi marehemu Johana Ng’eno akimtaja kama mwanasheria mahiri aliyetoa mchango mkubwa katika masuala ya kisheria ya Bunge.
Ichung’wa amesema Ng’eno alikuwa akishiriki kikamilifu katika mashauri ya kisheria, akiwashauri mawakili waliokuwa wakilitetea Bunge mahakamani kuhusu namna bora ya kuendeleza hoja zao.
Ichung’wa ameongeza kuwa historia ya mageuzi katika sekta ya makazi haitakamilika bila sura maalum kumhusu Johana Ng’eno
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































