#Local News

PVK YAKOSOA GHASIA ZA UCHAGUZI

Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya PVK umeonya kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu ujao jinsi ilivyoshuhudiwa kwenye chaguzi ndogo wiki jana, iwapo taasisi husika hazitachukua hatua madhubuti.

Kwenye kikao na wanahabari, mwenyekiti wa muungano huo Apostle Peter Manyuru ambaye ni kiongozi wa kanisa la JTM, ametoa wito kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwachukulia hatua kali viongozi wa kisiasa wanaochochea vurugu.

Aidha, ameitaka idara ya usalama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *