NYARIBO ATIMULIWA
Gavana wa kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo ametimuliwa mamlakani na wawakilishi wadi ambaowanadai gavana huyo anatumia mamlaka vibaya na ukiukaji wa katiba .
Wawakilishi wadi wa kaunti ya Nyamira wamemtimua gavana baada ya kupiga kura 23 kati ya 31 kumuondoa afisini kwa madai ya kutumia afisi yake visivyo ikiwa ni mara yake ya tatu hoja hiyo kujadiliwa katika bunge la kaunti hiyo.
Kutimuliwa kwake kunajiri baada ya msako wa tume ya kupambana na ufisadi EACC kuhusu uchunguzi wa millioni 382 za ufisadi kufuatia ununuzi ambao haukufuata sheria.
Imeandaliwa na Shadrack Maina
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































