RUTO AWATAKA VIJANA KUKUMBATIA NYOTA
Rais William Ruto amewahimiza vijana kote nchini kukumbatia mipango ya ujasiriamali inayoendeshwa na serikali kama vile mradi wa NYOTA, kama njia mojawapo ya kuimarika kiuchumi.
Akizungumza mjini Kisii wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwa vijana kutoka kaunti ya Kisii, Migori na Nyamira , Rais Ruto amesema mradi huo ni sehemu ya ahadi zilizotolewa na serikali yake kwenye kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Naye naibu wake Kithure Kindiki akiwatahadharisha vijana dhidi ya kutumiwa kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































