KAIMOSI TTC WAWANIA UBINGWAWA MPIRA WA WAVU KANDA YA MAGHARIBI
Kocha wa timu ya mpira wa wavu ya Chuo cha Ualimu cha Kaimosi Geoffrey Lwangu amesema analenga kutwaa ubingwa wa kanda ya Magharibi huku mashindano hayo yakianza katika eneo la Lugari, kaunti ya Kakamega.
Lwangu ameonyesha imani na uwezo wa kikosi chake kushinda wapinzani wao wakuu Bondo TTC, ambao waliwashinda kwa seti 3-2 katika fainali za mwaka uliopita.
Akizungumza baada ya kukamilisha maandalizi ya mwisho, Lwangu amesema timu yake imeimarisha maeneo muhimu kama kupokea mpira na kuzuia mashambulizi. Kaimosi TTC, inayoiwakilisha Kaunti ya Vihiga pamoja na Bunyore TTC, inalenga kupeperusha vyema bendera ya kaunti hiyo katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































