#Football #Sports

WACHEZAJI WA ALGERIA ZIDANE NA BELGHALI WAPIGWA MARUFUKU.

Wachezaji wa Algeria, Luca Zidane na Rafik Belghali, wamepigwa marufuku ya mechi mbili na nne mtawalia kutokana na kuhusika katika matukio mabaya yaliyojitokeza baada ya kupoteza kwa robo fainali dhidi ya Nigeria katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo ilitolewa na Shirikisho la Soka la Algeria (FAF), ambalo pia liliadhibiwa faini ya dola 100,000 kutokana na upungufu wa usalama na mwenendo usiofaa wa wachezaji, maafisa na mashabiki.

Mlinda mlango Zidane na beki Belghali watatumia marufuku yao wakati wa mchuano wa kufuzu kwa mashindano ya 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

WACHEZAJI WA ALGERIA ZIDANE NA BELGHALI WAPIGWA MARUFUKU.

CHELSEA WAJIWEKA VYEMA UCL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *