KAMISHNA WA MAGEREZA AWATAKA MAAFISA KUZINGATIA USALAMA
Kamishna Mkuu wa Magereza Patrick Aranduh amewataka maafisa wa magereza nchini kuzingatia kikamilifu taratibu za usalama, akisema jukumu lao kuu ni kuwafungia wafungwa kwa usalama na kulinda wananchi.
Akizungumza na wakurugenzi, makamanda wa kanda na maafisa wanaosimamia vituo vya magereza katika mkutano uliofanyika Chuo cha Mafunzo cha Maafisa wa Magereza, Aranduh ameonya kuwa uzembe au kupuuza taratibu za usalama hakutavumiliwa.
Aranduh ametoa wito wa uwajibikaji na kujituma zaidi, akisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa wafungwa na uendeshaji mzuri wa vituo vya kurekebisha tabia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































