OWALO AJIUZULU
Naibu mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu anayesimamia kitengo cha ufanikishaji wa utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza Eliud Owalo, amejiuzulu baada ya kutangaza azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Kupitia taarifa, Owalo amesema haiwezekani kwake kuendelea kuitumikia serikali ya Rais William Ruto baada yake kutangaza kuwania wadhifa huo.
Kulingana na Owalo, ni wakati wake pia kujipima nguvu katika kinyang’anyiro cha urais.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































