WETANG’ULA, JEN. MUHOOZI WAZUNGUMZIA MIGINGO
Suala la kuhangaishwa kwa wavuvi wa Kenya katika kisiwa cha Migingo Ziwani Victoria na vikosi vya usalama vya Uganda limepewa kipaumbele katika mkutano wa maspika wa mabunge ya Afrika Mashariki na mkuu wa jeshi la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba.
Haya ni kwa mujibu wa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, akisema Jenerali Muhoozi amekiri kuwepo kwa changamoto hizo, na kwamba litajadiliwa na serikali zote 2 kupata mwafaka.
Kupitia taarifa, Wetang’ula amesema amesisitiza haja ya usawa katika ugavi wa raslimali za pamoja katika Ziwa hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































