#Basketball #Sports

VIKOSI VYA AWALI VYA DEAFLYMPICS VYAONDOKA NCHINI

Vikosi vya mchezo wa handiboli na vikapu vimeondoka nchini kuelekea Japan kwa mashindano ya wanamichezo wasio na uwezo wa kusikia ya Deaflympics yatakayoandaliwa jijini Tokyo kuanzia kesho.

Timu ya handiboli ya wanaume iliondoka jana asubuhi huku ile ya wanawake ya vikapu ikiondoka kwa awamu 2, mchana na jioni.

Manahodha wa vikosi vyote wameelezea matumaini ya vikosi vya kufanya vyema kwenye mashindano hayo, matarajio yao yakisisitizwa na meneja wa kikosi cha wanawake ya vikapu Mary Chepkoi.

Kikosi cha handiboli ndicho kikosi cha kwanza kutoka nchini kuanza majukumu yao, kikiratibiwa kuchuana na Serbia katikia Group B Jumapili 6pm, kundi linalojumuisha mabingwa watetezi Croatia na Ufaransa.

Kenya pia itashiriki riadha, gofu na uaogeleaji katika mashindano hayo yatakayokamilika tarehe 26 mwezi huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

VIKOSI VYA AWALI VYA DEAFLYMPICS VYAONDOKA NCHINI

EACC: VUNJILIA MBALI TRAFIKI FISADI

VIKOSI VYA AWALI VYA DEAFLYMPICS VYAONDOKA NCHINI

EAGLES WA NIGERIA WAPAA HADI FAINALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *