#Local News

MAAFISA 4 NYAMIRA KUSHTAKIWA NA UFISADI

Maafisa 4 wakuu katika serikali ya kaunti y Nyamira wanatarajiwa mahakamani hii leo kufunguliwa mashtaka ya ufisadi baada ya kukamatwa hapo jana na maafisa wa tume ya kukabili ufisadi EACC.

Mkurugenzi wa idara ya nyumba Lameck Machuki, mwezake wa barabara Peris Muse, afisa mkuu wa fedha Assanet Maube na mwenzake wa barabara Josphat Oruru walikamatwa kwenye operesheni ya hapo jana katika makazi yao na ya gavana Amos Nyaribo.

EACC inasema imepata stakabadhi muhimu kusaidia katika uchunguzi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *