#Football #Sports

MZUNGUKO WA MWISHO KUELEKEA RAUNDI YA 16 UEFA

Mkondo wa mwisho wa kufuzu raundi ya 16 katika dimba la klabu bingwa bara Ulaya unasakatwa wiki hii, jumla ya mechi 8 zikisakatwa leo na kesho usiku.

Katika pambano moja, Atletico Madrid watakuwa na kibarua cha kutegua msongamano dhidi ya Club Brugge, kufuatia sare ya mabao 3-3 katika mkondo wa kwanza, timu zote 2 zikiwa na nafasi sawa za kufuzu raundi ya 16 ila Atletico wanajivunia mashabiki wa nyumbani.

Wakati uo huo, kibarua cha pekee kwa Newcastle kitakuwa ni kulinda uongozi wao wa mabao 5 kutokana na ushindi wa mabao 6-1 ugenini dhidi ya mabingwa wa Azerbaijan, Qarabag FK.

Hali sawa itakuwa kwa Bayer Leverkusen, ambao wanacheza nyumbani wakiwa tayari mabao 2 mbele kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Olympiacos wiki jana.

Nao waangusha miamba- Bodo/Glimt wa Norway, watalenga kuwabomea kabisa miamba wa Italia Inter Milan, watakapocheza mechi yam kondo wa pili leo usiku.

Glimt walivuna ushindi wa mabao 3-1 nyumbani, na kibarua leo ni kuhakikisha wanavuruga mechi na kuwatatiza miamba hao ili kulinda uongozi wao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MZUNGUKO WA MWISHO KUELEKEA RAUNDI YA 16 UEFA

SESKO AWEKA HAI MATUMAINI YA UNITED UEFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *