WAHADHIRI WASISITIZA MASOMO HAYAPO VYUONI
Wizara ya elimu na wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma kwa mara nyingine wamekosa mwafaka kuhusu mgomo wa wahadhiri hao, ambao wamepinga ripoti ya wizara ya elimu kwamba masomo yamerejelewa katika baadhi ya vyuo vikuu vya umma.
Viongozi wa muungano wa UASU wamesisitiza kuwa masomo yamelemazwa katika vyuo vikuu vyote vya umma na kwamba mgomo huo utaendelea hadi matakwa yao yatakapoangaziwa na serikali.
Wanafunzi katika chuo kikuu cha TUK pia wamepinga madai ya serikali kwamba masomo yanaendelea chuoni humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































