WAAKAZI WALALMIKIA UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU MAKONGENI.
Zaidi ya wakaazi 3,000 wa mtaa wa Makongeni hapa jijini Nairobi Nairobi wamelalamikia ubomoaji unaoendelea ili kupisha kujengwa kwa nyumba za bei nafuu kwenye ardhi ya ekari 139.
Hata hivyo baadhi ya wakaazi wamelalamikia fidia duni ambayo wanalipwa wakisema fedha hizo hazitoshi kugharamia mahitaji yao huku wengine wakiwa na tumbo joto ya masomo ya wanao mwaka ujao.
Aidha ni Zoezi ambalo linaendeshwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi,serikali ikisisistiza kuwa nyumba za bei nafuu ndio njia mwafaka na suluhu kwa wananchi kupata makaazi bora.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































