KIPKOSGEI BINGWA WA DUNIA RASMI
Chipukizi wa Kenya Phanuel Kipkosgei Koech, amepata afueni baada ya shirikisho la riadha ulimwenguni kuidhinisha rekodi yake katika mbio za mita 1,500 kwa wanaume za Paris Wanda Diamond League mwezi Juni mwaka jana.
Akiwa na umri wa miaka 18 wakati huo, Kipkosgei aliandikisha muda wa dakika 3:27.72 akimaliza nyuma ya Azeddine Habz na kuvunja rekodi ya dunia ya dakika 3:28.81 ya Mkenya Ronald Kwemoi aliyoiandikisha mwaka 2014 jijini Monaco katika mbio hizo kwa wanariadha walio chini ya umri wa miaka 20.
Hatua hiyo pia ilimworodhesha kinda huyo kwenye nafasi ya 9 ya dunia, ikiwa ni hatua kubwa zaidi kwake ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya pili kushiriki mbio hizo za mita 1,500.
Lich aya kutoanya vizuri katika mashindano ya 2025 World Championships jijini Tokyo, Japan ambako alitekwa katika mzunguko wa mwisho na hivyo kukosa nusu fainali, kinda huyo atategemewa pakubwa katika mbio za 2026 Diamond League zitakazoanza siku 99 zijazo jijini Doha Qatar.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































