WINNIE ODINGA: VIONGOZI WANATISHWA
Mwanawe kinara mwanzilishi wa chama cha ODM marehemu Raila Odinga, Winnie Odinga, amekosoa jinsi mabadiliko ya uongozi wa chama hicho yalitekelezwa baada ya kifo cha Odinga, akiwashtumu baadhi ya viongozi kwa madai ya kuwatenga wanachama walio na mtazamo kinzani, mbali na ukiukaji wa katiba ya chama.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga usiku wa kuamkia leo, Winnie amesema chama hicho kilishindwa kuwasiliana kwa uwazi, na kuruhusu viongozi wachache kutoa mwelekeo muhimu wa chama.
Amependekeza kuandaliwa kwa kongamano la kitaifa la wajumbe ili kutatua migogoro chamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































