#Local News

WASHUKIWA 7 WA VURUGU KARIOBANGI WAKAMATWA

Idara ya polisi imethibitisha kuwakamata watu 7 wanaohusishwa na vurugu zilizoshuhudiwa katika kanisa moja mtaani Kariobangi North jijini Nairobi wakati wa ibada iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.

Kupitia taarifa, idara hiyo imesema washukiwa Charles Opiyo, Wilson Okoth, Michael Mutunga, Reggy Opiyo, Brian Omondi, Gordon Onyango na Elisha Ochieng wamekamatwa mtaani Lucky Summer.

Uchunguzi katika vurugu hizo unaendeshwa na kamanda wa polisi eneo la Nairobi na mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WASHUKIWA 7 WA VURUGU KARIOBANGI WAKAMATWA

WAKENYA HAWATAKI MAHAKAMA, WADAU

WASHUKIWA 7 WA VURUGU KARIOBANGI WAKAMATWA

PAMBANO LA GOR- BANDARI LAHAMISHWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *