PENGO LA UJUZI LASHUHUDIWA KATIKA HAZINA NA BUNGE
Kenya inakabiliwa na ongezeko la mzigo wa madeni ambao unafikia asilimia 65 ya pato la taifa, mbali na kiwango cha juu cha sasa cha asilimia 55. Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Hazina na Bunge zinahusika kwa kiasi fulani.
Katika ripoti iliyopewa jina la Unpacking the Drivers of Public Debt Dynamics in Kenya, Benki imetilia shaka uwezo wa Bunge wa kutathmini hali ya madeni ya nchi. Ripoti hiyo, ambayo imeandaliwa Duncan Ouma wa AfDB na mkuu wa utafiti Martin Nandelenga, imeonyesha kuwa kulikuwa na upungufu katika Ofisi ya Usimamizi wa Madeni ya Umma katika Hazina ya Kitaifa ambayo imechangia deni la umma kupanda hadi viwango vya juu zaidi.
Hata hivyo, mkurugenzi wa Ofisi ya Bunge ya Bajeti, ofisi ambayo iliundwa mwaka 2007 kusaidia wabunge kufuatilia bajeti ya taifa, amesema kuwa ofisi hiyo ina uwezo wa kutosha.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































