WIZARA YA ELIMU YAZUIA MGAO KWA SHULE 29
Shule 29 zitasubiri kwa muda usiojulikana kabla ya kupokea mgao wa serikali kutokana na uchunguzi unaoendelea ili kuondoa shule na wanafunzi hewa kwenye orodha ya wizara ya elimu.
Akizungumza akiwa mbele ya kamati ya elimu katika bunge la kitaifa, Waziri wa elimu Julius Ogamba amesema wizara hiyo imezuia mgao wa fedha kwa shule hizo baada ya matatizo kuibuka wakati wa ukaguzi.
Kamati hiyo hata hivyo imeikosoa wizara ya elimu kwa kuruhusu shule hizo kuwasajili watahiniwa ilhali hazijapokea mgao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































