HASARA, MAAFA YA MAFURIKO
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini imethibitishwa kufikia 66 huku maelfu ya wengine wakiendelea kukadiria hasara, idara ya polisi ikisema zaidi ya watu 2,000 wamehamishwa na mafuriko kwa lazima.
Jijini Nairobi, usimamizi wa mradi wa uimarishaji wa Nairobi River umeorodhesha sehemu 37 kama zilizo kwenye hatari ya kufurika, wakazi wakitakiwa kuchukua tahadhari wakati huu wa masika.
Baadhi ya maeneo hayo ni South B na South C, Kibra, Kilimani, Kariobangi, Kiambiu, Dandora, Industrial Area na katikati mwa jiji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































