UFADHILI MDOGO WAONGEZA MADAI YA FIDIA
Maelfu ya wakenya walioathirika katika migogoro kati ya wanyamapori na binadamu wanaendelea kuteseka kutokana na uchelewashaji wa mara kwa mara na ufadhili mdogo, hatua ambayo imechangia ongezeko la madai ya fidia inayotokana na migogoro hiyo.
Akiwa mbele ya kamati ya uhasibu bungeni, katibu mkuu katika idara ya wanyamapori Silvia Museiya, amesema licha ya sheria inayoongoza fidia hiyo kuwapo tangu mwaka 2013, ufadhili wa kufanikisha fidia hiyo ulianza kutolewa mwaka 2017.
Kamati hiyo hata hivyo imetaka madai hayo kulipwa kisheria bila kucheleweshwa, huku ikiibua malalamishi kuwa malipo yanayoripotiwa na matukio halisi mashinani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































