#Local News

KAMATI YA KIUFUNDI KUFANIKISHA MAZUNGUMZO YA UDA-ODM

Mazungumzo ya ushirikiano wa kisiasa kati ya vyama vya UDA na ODM kuelekea uchaguzi mkuu ujao yatafanikishwa na kamati ya kiufundi yenye wanachama 8.

Haya yamependekezwa na Rais William Ruto, akizungumza baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa ajenda 10 zilizoafikiwa baina ya vyama hivyo mwaka jana, na kusema kuwa ripoti ya kamati hiyo itawasilishwa kwa vinara wa vyama hivyo kabla ya uamuzi wa mwisho.

Amesisitiza kwamba serikali jumuishi itapitisha miswada muhimu kutokana na idadi kubwa ya wabunge na maseneta.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *