MARIGA ASEMA STARLETS WANA UWEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2027
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF), McDonald
Mariga, anaamini kwamba timu ya taifa ya wanawake Harambee
Starlets ina uwezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake
mwaka 2027 nchini Brazil, kufuatia uchezaji wao mzuri katika
hatua za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON).
Starlets walifuzu baada ya kuichapa Gambia kwa jumla ya
mabao 4–1 kwenye raundi ya mwisho ya kufuzu — ushindi wa
3–1 nyumbani na 1–0 ugenini nchini Senegal.
Mariga amesema maandalizi kabambe yanaendelea kuhakikisha
Starlets wanakuwa tayari kwa mashindano ya bara Afrika, na
hatimaye kufanikisha ndoto ya kushiriki Kombe la Dunia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































