IEBC YAPOKEA VIFAA VYA CHAGUZI NDOGO
Usambazaji wa vifaa vyote vya uchaguzi mdogo katika maeneo mbali mbali nchini utaanza hapo kesho, baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kupokea shehena ya kwanza ya vifaa hivyo vilivyotayarishwa nchini Ugiriki.
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa JKIA, mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, amesema shehena nyingine inatarajiwa nchini hii leo, huku akilalamikia gharama ya juu na muda mrefu unaochukuliwa kutayarisha vifaa hivyo nchini Ugiriki kutokana na ukosefu wa uaminifu kwa wachapishaji wa humu nchini.
Uchaguzi huo utaandaliwa Alhamisi wiki ijayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































