WAGONJWA TAABANI NAIROBI
Huduma za matibabu katika hospitali za umma jijini Nairobi zinatarajiwa kutatizika zaidi kutokana na mgomo wa madaktari na maafisa wa kliniki ambao umeingia siku ya 4, huku wauguzi wakitarajiwa kujiunga na mgomo huo kuanzia leo.
Madaktari na maafisa kliniki wamesusia kazi ili kuishinikiza serikali ya kaunti ya Nairobi kuwapa malipo yao ya kati ya mwezi 1-3, wakimshutumu gavana Johnson Sakaja kwa madai ya kuwapuuza.
Maafisa wa kliniki wamekuwa kwenye mgomo tangu Disemba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































