#Local News

WIZARA YA AFYA YAANZISHA UCHUNGUZI KUHUSU KIFO MUKUMU

Wizara ya Afya imeanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mama mjamzito kilichotokea katika hospitali ya kimisheni ya Mukumu, Kaunti ya Kakamega.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge, Waziri wa Afya Aden Duale amesema wizara inafuatilia chanzo cha kifo cha Grace Wambui Misigo baada ya familia kudai kuwa wauguzi katika hospitali hiyo walimdhulumu wakati wa kujifungua hadi akafariki.

Waziri Duale amesema uchunguzi wa kina utafanyika ili kubaini ukweli na hatua stahiki zichukuliwe.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

WIZARA YA AFYA YAANZISHA UCHUNGUZI KUHUSU KIFO MUKUMU

MBUNGE MANYATTA AMKOSOA WAZIRI WA USALAMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *