SERIKALI YAONGEZA BIMA YA SARATANI HADI SHILINGI 800,000
Waziri wa Afya Aden Duale amesisitiza dhamira ya serikali katika kuboresha upatikanaji wa matibabu ya saratani kwa kuongeza kifurushi cha matibabu chini ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF) kutoka shilingi 500,000 hadi 800,000.
Akizungumza katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Coast General kaunti ya Mombasa Duale amesema serikali itagharamia mikataba ya huduma ili kuhakikisha mashine za matibabu ya saratani zinahudumiwa na kufanya kazi ipasavyo.
Kwa upande wake, Gavana wa Kaunti ya Mombasa Abdulswamad Nassir ameahidi kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa wodi maalum ya saratani katika hospitali hiyo, hatua inayolenga kuimarisha huduma kwa wagonjwa wa saratani katika ukanda wa Pwani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































