KCSE 2025: WATAHINIWA 1,180 WAKOSA MATOKEO
Huku sherehe zikiendelea kuhusiana na matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka 2025, watahiniwa 1,180 hawana cha kufurahia baada ya wizara ya elimu kufutilia mbali matokeo yao kwa madai ya kuhusika na udanganyifu kwenye mtihani huo.
Akizungumza katika shule ya AIC Chebisas kaunti ya Uasin Gishu wakati wa kutangaza matokeo hayo, Waziri wa elimu Julius Ogamba amesema uamuzi huo umeafikiwa baada ya uchunguzi ulioanza mwezi Novemba mwaka jana kukamilika.
Aidha, ameweka wazi jinsi watahiniwa wa mwaka jana watapokea matokeo yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































