GOR WATANGAZA KUREJEA
Mshikilizi wa rekodi ya ubingwa wa ligi kuu ya FKF Premier League Gor Mahia wamepanda hadi nafasi ya 2 katika jedwali la ligi hiyo baada ya kuwazamisha Mathare United kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Kasarani hapo jana.
Gor waliendeleza msururu wa matokeo bora msimu huu, wakiwa wameshinda mechi 4 mfululizo licha ya kuanza msimu kwa kichapo.
Baada ya kichapo dhidi ya Bidco kwenye mechi ya ufunguzi, mabingwa hao mara 21 walijikusanya na kutangaza ubabe wao, wakipata ushindi dhidi ya Sofapaka, KCB, Posta Rangers na Mathare, wakiwa na alama 12, alama 1 pekee nyuma ya viongozi Kakamega Homeboyz.
Gor Mahia kadhalika wana mechi 1 mkononi dhidi ya Homeboyz.
Katika mechi yah apo jana, Shariff Musa na nguvu mpya Bryson Wangai walifunga mabao hayo na kuihakikishia Gor ushindi huo.
Katika mechi nyingine ya hapo jana, Murang’a Seal walitoka nyuma na kuzichana barua za Posta Rangers kwa kulazimisha sare ya mabao 2.
Mchezaji wa zamani wa AFC Leopards Caleb Olilo aliwaweka wanabarua mbele katika dakika ya 24 kabla ya Faustin Odhiambo kuongeza uongozi dakika 11 baadaye.
Hata hivyo, mabao Murang’a Seal walizirarua barua dakika ya 67 na 75 kupitia kwa Joe Waithira.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































