#Football #Sports

DROO YA ROBO FAINALI CAF CONFEDERATIONS CUP

Debi la Morocco ndilo gumzo kubwa katika awamu ya robo fainali ya dimba la mashirikisho, CAF Confederations Cup msimu wa 2025-26, kufuatia droo iliyofanyika hapo jana nchini Misri.

Olympique de Safi watakuwa wenyeji Wydad Casablanca kwenye mkondo wa kwanza wa robo fainali hiyo, katika pambano la timu zinazofahamiana vyema na litakalohakikisha kuwa Morocco ina mwakilishi katika awamu ya semi fainali.

Miamba wa soka nchini Misri Zamalek SC, wataanza kampeni yao ya kuingia nusu fainali ugenini dhidi ya AS Otoho ya Congo katika mkondo wa kwanza wa robo fainali.

Klabu nyingine ya Misri, Al Masry, itaialika CR Belouizdad kutoka Algeria, nayo AS Maniema ya DR Congo ikiikaribisha Union Sportive de la Madeina d’Alger maarufu kama USM Alger wa Algeria katika mechi za ufunguzi za robo fainali.

Mechi hizo zote zitachezwa wikendi ya tarehe 13-15, na marudiano wikendi ya tarehe 20-22 mwezi ujao, huku semi fainali zikisakatawa katika kipindi sawa mwezi Aprili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DROO YA ROBO FAINALI CAF CONFEDERATIONS CUP

AZMA YA GSU LIGI YA KVF INAPORUDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *