NDINDI NYORO AHOJI UUZAJI WA MALI ZA UMMA
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesisitiza haja ya kuimarishwa kwa uwajibikaji wa kifedha, huku akipinga mpango wa serikali wa kubinafsisha Kampuni ya Kenya Pipeline na kuuza asilimia 15 ya hisa zake katika kampuni ya Safaricom.
Akizungumza katika Kongamano la 34 la Kiuchumi lililofanyika jijini Nairobi, Nyoro ametaka serikali kuweka wazi maelezo kuhusu mpango wa uuzaji wa kampuni za umma.
Aidha Nyoro amesisitiza kuwa ni lazima fedha zitakazopatikana kutokana na uuzaji huo zitumike kwa manufaa ya wananchi na si kwa maslahi ya wachache.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































