#Football #Sports

KOCHA MPYA WA POLICE FC AAHIDI KUREJESHA UBABE KLABUNI

Kocha mpya wa Police FC, Dusan Stojanovic, ameapa kurejesha
ubabe wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) na
kujenga kikosi chenye uwezo wa kushindana na vilabu vikubwa
barani Afrika.
Mtaalamu huyo raia wa Serbia alitambulishwa rasmi Jumapili
jioni katika Uwanja wa Police Sacco, muda mfupi baada ya kikosi
chake kutoka sare tasa ya 0–0 dhidi ya Posta Rangers.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na wanahabari,
Stojanovic alionyesha matumaini kuhusu mwelekeo wa klabu
hiyo na kusisitiza kwamba misingi ya mafanikio yake itajengwa
juu ya bidii, umoja na nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KOCHA MPYA WA POLICE FC AAHIDI KUREJESHA UBABE KLABUNI

GUARDIOLA  ALAUMU WAAMUZI WA EPL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *