WANNE WAFARIKI KWENYE MAANDAMANO CAMEROON
Watu wasiopungua 4 wameuawa kwenye maandamano katika kitovu cha uchumi jijini Douala nchini Cameroon huku baraza la kikatiba likijiandaa kutangaza matokeo ya urais hii leo.
Kulingana na msimamizi wa eneo hilo Samuel Dieudonne Diboua, vituo vya polisi wamevamiwa na waandamanaji walio wafuasi wa mwaniaji wa upinzani Issa Tchiroma, na polisi walilazimika kutumia nguvu ili kujilinda.
Wafuasi wake walikiuka agizo la kuwazuia kuandamana katika miji kadhaa, huku Tchiroma akishikilia kuwa alimshinda Rais Paul Biya kwenye uchaguzi wa tarehe 12 mwezi huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































